Rwanda yaanza maandalizi ya Uchaguzi Mkuu Julai 15 kumchagua rais na wabunge
Manage episode 423207398 series 1091037
Wananchi wa Rwanda wanajiandaa kupiga kura tarehe 15 mwezi Julai kumchagua rais na wabunge.
Wiki iiyopita, Tume ya Uchaguzi ilitangaza orodha ya awali ya wagombea urais ambao ni rais Paul Kagame ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 1994, Frank Habineza kutoka chama cha Democratic Green na Philippe Mpayimana mgombea binafsi.
Mwanasiasa na mpinzani wa Kagame, Diane Rwigara, kutoka chama cha People Salvation Movement, ombi lake lilikataliwa.
Tunachambua maandalizi ya uchaguzi nchini Rwanda. Wachambuzi wetu ni Edwin Kegoli akiwa Nairobi na Mali Ali akiwa jijini Paris
24 episode